Dodoma FM

Manda, Ilangali watembea umbali mrefu kusaka mtandao

30 July 2025, 1:20 pm

Wananchi hao wanasema kukosekana kwa mtandao kunawalazimu kutembea umbali mrefu au kufanya mawasiliano nyakati za usiku.Picha na Ucsaf.

UCSAF imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanapata huduma bora za mawasiliano.

Na Victor Chigwada.
Ikiwa Sera ya Mawasiliano inabainisha kuwa wananchi wote wanapata huduma bora, salama, na nafuu za mawasiliano bila ubaguz,Hali ni tofauti kwa Wakazi wa vijiji vya Manda na Ilangali wilayani Chamwino ambao wanapitia changamoto ya ukosefu wa mawasiliano ya Simu na kuwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza kwa Nyakati tofauti wamesema wamekuwa wakipatia changamoto hasa wakihitaji huduma za dharura.

Wamesema hatua hiyo imewalizimu kufanya mawasiliano nyakati za Usiku.

Pia wananchi hao wamesema wameshindwa kuwasiliana na watoto wao waliopo shuleni.

Ikumbukwe kuwa Mpango wa mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF wa Kuboresha Mawasiliano Vijijini Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanapata huduma bora za mawasiliano,hasa katika maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara.
Uwekezaji huu unalenga si tu mawasiliano ya simu, bali pia kuimarisha kilimo, elimu, afya, na usalama kupitia upatikanaji wa taarifa kwa njia ya kidijitali.

Bado tunaendelea na juhudi za kutafuta Mamlaka ya Mawasiliano kwa wote kujua wanampango wa kutatua changamoto kwa wakazi wa vijiji vya Manda na Ilangali.