Dodoma FM

Wafanyabiashara wa chakula watakiwa kuzingatia usafi

22 July 2025, 3:55 pm

Picha ni Afisa Afya Mkoa wa Dodoma Shadrack Geofrey wakati akizungumza na Dodoma Tv.Picha na Farashuu Abdallah.

Afisa Afya Shadrack Geofrey ametoa wito kwa viongozi wa mitaa Dodoma kuwa na utaratibu wa kutembelea maeneo ya biashara ya chakula ili kujiridhisha juu ya mwenendo wa biashara hiyo kuwa ni safi na salama.

Na Farashuu Abdallah.

Wafanyabiashara wa Chakula Jijini Dodoma wameshauriwa kuzingatia usafi katika biashara zao ili kuepuka magonjwa yatokanayo na uandaaji mbaya wa chakula.

Ushauri huu umetolewa na Afisa Afya Mkoa wa Dodoma Shadrack Geofrey wakati akizungumza na Dodoma Tv amesema ni muhimu kwa wafanyabiashara wa chakula kuzingatia  usafi katika biashara hiyo ikiwemo unawaji wa mikono kwa maji safi na salama ,kufunika nywele na uwepo wa choo safi katika mazingira hayo.

Sauti ya Shadrack Geofrey .

Pia amesema kuwa ni vyema wafanyabiashara wafuate sheria na taratibu za uaandaaji wa chakula  ikiwemo kuwa na cheti kutoka TBS ambacho  kitamtambulisha na kumpa usalama  katika biashara ya chakula na kuongeza kuwa endapo mtu hatafuata taratibu za uandaaji wa chakula hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Awali nilizungumza na Wafanyabiashara wa Chakula pamoja na walaji ambapo wamesema licha ya kuzingatiwa usafi kwenye chakula kuwa inaepusha magonjwa, lakini pia wateja wengi wanavutiwa na hali ya usafi katika maeneo hayo.

Sauti ya Shadrack Geofrey .