Dodoma FM
Dodoma FM
22 July 2025, 2:23 pm

Ikumbukwe kuwa mradi wa ukarabati wa jengo la zahanati ya Ihumwa ulianza tarehe 10 /08/2023, ukigharimu kiasi cha shilingi milioni 235.9 fedha kutoka Shirika la Wahisani ABBOT.
Na Lilian Leopord.
Uboreshwaji wa miundimbinu uliofanyika katika zahanati ya Ihumwa iliyopo jijini Dodoma umesaidia wananchi kupata huduma bora na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito.

Akizungumza na Taswira ya habari Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Ihumwa, Aisha Abubakari wakati akilezea uboreshwaji uliofanyika katika zahati hiyo amesema wapokea vifaa vilivowasaidia vya kisasa ambavyo vimekua msaada mkubwa kwa wananchi.
Naye Berazel Kasuga ambaye ni Mkazi wa Ihumwa amesema uboreshaji wa zahanati hiyo umewasaidia wanawake na watoto ambao walikua wanapata changamoto ya kutembea za umbali mrefu kupata huduma za afya.