Dodoma FM
Dodoma FM
3 July 2025, 4:32 pm

Katika kuhitimisha ziara yake Wilayani Kondoa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka wananchi kuhakikisha wanashiriki katika Uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kupiga kura.
Na Seleman Kodima.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameutaka uongozi wa wakala wa majisafi na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA Wilayani Kondoa kuhakikisha inatutua changamoto ya kukosekana kwa kwa maji Bolisa.
Haya yanajiri kufuatia ziara aliyoifanya katika wilaya hiyo kata ya Bolisa Kondoa ambapo alifanya mkutano na wananchi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero zao.
Aidha katika mkutano huo Mhe. Senyamule alizindua nyumba ya walimu iliyopo katika Shule ya Bolisa na kuwataka walimu kuwa chachu ya maendeleo ya elimu.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kondoa Fatma Nyangasa amesema kukamilika kwa jengo hilo kutatatua changamoto ya makazi ya walimu katika shule ya bolisa.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alitembelea ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta EACOP mradi uliyopita wilaya ya Chemba na Kondoa na kusema kuwa mradi huo utatoa fursa za kiuchumi kwa wananchi.