Dodoma FM

Wanawezaje kuzishinda mila, desturi kupata nafasi za uongozi kisiasa?

25 June 2025, 10:54 am

Je, kwanini wanawake wanaathirika zaidi na mila kandamizi? Picha na Nukta habari.

Katika jamii nyingi, mila na desturi huwakosesha wanawake fursa ya kushiriki katika mchakato wa maamuzi iwe katika familia, kijiji au hata kwenye taasisi za kisiasa.

Karibu msikilizaji wa makala ya Amua inayoandaliwa na kutangazwa na Dodoma FM. Makala hii inakujia kila Jumapili kuanzia saa nane na nusu mchana hadi saa tisa kamili alasiri. Kukuletea makalahii mimi ni Mariam Kasawa na mwenzangu ni Mariam Matundu karibu.

Wiki hii katika makala ya Amua tunaangazia kuhusu mila na desturi kandamizi zinavyowakwamisha wanawake kuwania nafasi za uongozi.

Katika michakato ya uteuzi au uchaguzi, jamii huwa na upendeleo kwa wanaume kutokana na imani kuwa wao ni viongozi wa asili. Hii huwafanya wanawake kukosa uungwaji mkono hata kama wana sifa zinazostahili.