Dodoma FM
Dodoma FM
24 June 2025, 12:36 pm

Katika safari ya kutafuta elimu bora, bado kuna kundi la vijana ambao hupambana na changamoto za kiuchumi.
Na Mariam Kasawa
Serikali ya Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOSO) imezindua mfuko maalum wa kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kumudu gharama za masomo.
Katika safari ya kutafuta elimu bora, bado kuna kundi la vijana ambao hupambana na changamoto za kiuchumi, hali inayowafanya washindwe kufikia ndoto zao za kielimu.
Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali ya Wanafunzi ya chuo kikuu cha Dodoma UDOSO imeanzisha mfuko maalum wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wasio na uwezo, kama sehemu ya kuhimiza usawa na ujumuishwaji katika elimu ya juu kama anavyo eleza rais wa chuo hicho Bi. Jackline Humbaro.

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma nao unaunga mkono jitihada hizi ambapo Makamu mkuu wa chuo hicho Prof Lugano Kusiluka anasema hatua hii inafaa kuigwa na vyuo vingine nchin.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mfuko huo anasema Bi Carolyne Nombo Katibu mkuu wa wizara ya elimu ameipongeza serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodona UDOSO ambapo amesema viongozi hawa wana maono ya mbali ambayo yatawanufaisha wananfunzi na watanzania.