Dodoma FM
Dodoma FM
19 June 2025, 12:36 pm

Zoezi hilo lilienda sambamba na utoaji wa Vyeti kwa wanafunzi waliofanya Vizuri katika mashidano hayo.
Na Mariam Kasawa.
Uongozi wa Chuo kikuu cha Dodoma UDOM umewapongeza wanafunzi waliofanya Vizuri katika Mashindano ya Huawei ICT Global Competition 2025 yaliyofanyika nchini China mwaka huu 2025.
Akitoa Pongezi hizo Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma Prof.Lughano Kusiluka amesema ni Heshima kwa Chuo hicho pamoja na nchi kwa Ujumla kwa hatua ya Wanafunzi hao kupambana hadi kufanikiwa kushinda mashindano hayo.

Awali kaimu Rasi wa Ndaki wa Sayansi ya kompyuta na Elimu Angavu kutoka chuo kikuu cha Dodoma Dkt Florence Rashindi amebainisha hatua walizopita wanafunzi wa chuo hicho na Idadi waliotoa katika ushiriki wa mashindano hayo kwa Mwaka 2025.
Sigrid Nyaki ni miongoni mwa washindi kutoka Chuo hicho amesema bado wanasafari ndefu ya kufika mafanikio kama hayo hivyo ametoa rai kwa wanafunzi wengi kuamini inawezekana iwapo wataweka bidii.
Aidha katika tukio lililoandaliwa na Chuo hicho kwa ajili ya kuwapongeza wanafunzi hao lilienda sambamba na utoaji wa Vyeti kwa wanafunzi waliofanya Vizuri katika mashidano hayo akiwemo Sigfrid Nyaki,Paul Nkingwa,Felix Kuluchumila,na Godlove Hipolite.