Dodoma FM

Serikali yaahidi kuendelea kutumia tafiti za vyuo vikuu

17 June 2025, 3:28 pm

Picha ni mgeni rasmi Bw. Wilson Charles Mahera Naibu katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na Teknolojia akimuwakilisha Naibu waziri mkuu katika kongamano hilo .Picha na Chuo kikuu cha Dodoma.

Kongamano lapili la sayansi ya Afya chuo kikuu cha Dodoma linafanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa jiji Mtumba ambapo kaulimbiu ya mwaka huu inasema Evidence based practise and innovation in addres heaith challenges.

Na Mariam Kasawa.

Serikali kupitia wizara ya Afya imesema itaendelea kushirikiana na vyuo vyote Nchini pamoja na kutumia tafiti zinazo fanywa na vyuo vikuu hususani katika sekta ya Afya.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace magembe alipo kuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa kongamano lapili la sayansi ya Afya Chuo kikuu cha Dodoma ambapo amesema wizara ya Afya itatumia tafiti mbalimbali zinazo fanya na vyuo vikuu hapa nchini.

Sauti ya Dkt. Grace Magembe.
Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma Lugano Kusiluka akiongea katika kongamano hilo.Picha na Chuo kikuu cha Dodoma.

Nae makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma Lugano Kusiluka anasema lengo la kongamano hilo ni kubadilishana uzoefu na kuchangia mawazo kutoka kwa wataalamu mbalimbali na kuyarejesha kwa jamii.

Sauti ya Lugano Kusiluka

Akimuwakilisha Naibu waziri Mkuu na waziri wa nishati Dkt. Dotto Biteko katika kongamano hilo mgeni rasmi Bw. Wilson Charles Mahera amesema vyuo vikuu nchini vina wajibu wa kuibua changamoto zinazo ikabili sekta ya Afya.

Sauti ya Wilson Charles Mahera.