Dodoma FM

Wananchi Gendabi mbioni kunufaika na mradi wa maji wa bilion 1.2

5 June 2025, 3:36 pm

Picha ni viongozi hao wakikagua miundombinu ya mradi huo wa maji.Picha na Kitana Hamis.

Takribani wananchi 5,000 wa vijiji vitano katika kata hiyo wanatarajia kunufaika na mradi huo wa maji.

Na Kitana Hamis.
Takribani wananchi 5,000 kutoka vijiji vitano vya Kata ya Gendabi, Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, wanatarajiwa kunufaika na mradi wamaji unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.2, baada ya miundombinu ya awali kuharibiwa na maporomoko ya tope na mawe kutoka Mlima Hanang mwishoni mwa mwaka2023.

Akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Hanang, Eng. Felix Molel, amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kumaliza changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa maji safi nasalama kwa wakazi wa eneo hilo.

Picha ni ramani ya vijiji hivyo vitakavyo nufaika na mradi huo wa maji.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA, Mhandisi Ruthi Koya, amepongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo, akieleza kuwa ni ishara ya dhamira ya kweli ya serikali katika kuwafikia wananchi vijijini kwa huduma zamsingi.

Habari kamili.