Dodoma FM

‘Mita tano usafi wangu, usafi wangu mita tano’ kuzingatiwa

3 June 2025, 2:46 pm

Wakazi wa kata ya Kikuyu Kusini wakifanya usafi katika mitaro iliyopo katika mtaa huo.Picha na Lilian Leopord.

Kilele cha wiki ya Mazingira Duniani hufanyika Juni 05 kila mwaka ambapo mwaka huu kaulimbiu ya siku ya mazingira ni mazingira yetu na Tanzania ijayo tuwajibike sasa dhibiti matumizi ya plastiki.

Na Mariam Kasawa.

Wakazi wa jiji la Dodoma wamehimizwa kuzingatia na kudumisha kampeni ya mita tano usafi wangu ili kuendelea kuweka jiji la Dodoma katika hali ya usafi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha usafi na udhibiti wa taka Dickson Kimaro aliposhiriki usafi katika kata ya kikuyu kusini ikiwa ni katika kuadhimisha wiki ya mazingira duniani jun 1 hadi Juni 5 mwaka huu.

Sauti ya Bw. Dickson Kimaro.

Baadhi ya wananchi wa kikuyu kusini walioshiriki katika zoezi la kufanya usafi wamesisitiza  kuwa usafi unaanza kwa mtu mmoja mmoja hivyo ni muhimu kila mmoja kutimiza jukumu hilo.

Sauti za wananchi