Dodoma FM
Dodoma FM
20 May 2025, 3:53 pm

Wananchi wanadai kuwa changamoto hii imeshindwa kupatiwa ufumbuzi.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa vitongoji vya malechela ,Lusinde na sokoine Kijiji Cha Mnase wameendelea kulia na changamoto ya kukosekana kivuko baina ya wananchi na reli ya mwendokasi(SGR)
Wakieleza namna changamoto hiyo ambavyo imekuwa ikiwaathili hususani watoto wadogo wanapo hitaji kuvuka kwenda shuleni pamoja na wajawazito na wagonjwa mbalimbali wanapo hitaji huduma za afya
Aidha wamesema kuwa changamoto hiyo ya kutokuwepo Kwa kivuko rasmi imekuwa ikipelekea kutumia njia za makalavati ya maji ili kuvuka eneo hilo jambo ambalo limewaathili wanafunzi hususani wa umri mdogo pindi wanapokutana na maji kwenye makaravati
Wakizungumza na taswira ya habari wameiomba Serikali kuingilia kati changamoto hiyo kwani mkandarasi wa mradi imekuwa ni muda mrefu ameshindwa kutelekeza ujenzi wa kivuko
Ayubu Malima mwenyekiti kutoka vitongoji hivyo amekiri uwepo wa adha hiyo ambayo imeshindwa kupata suluhu tangu kuanza Kwa maradi wa ujenzi wa reli hata sasa