Dodoma FM
Dodoma FM
14 May 2025, 4:18 pm

Ili kuwepo na tija katika sekta ya utaalii nanchi iweze kuongeza pato la taifa ni vema serikali ikaweka mazingira rafiki.
Na Farashuu Abdallah.
Baadhi ya wadau wa masuala ya utalii wameshaur kuwepo na punguzo la tozo katika taasisi binafsi zinazo shughulikia sekta ya maliasiri na utalii hapa nchini.
Wakizungumza na kituo hiki wadau hao wanaoshughulika na masuala ya uongozaji wa utalii wamesema ili kuwepo na tija katika sekta ya utaalii nanchi iweze kuongeza pato la taifa ni vema serikali ikaweka mazingira rafiki hususani katika tozo zinazotozwa katika taasisi hizo zinazowaleta watalii hapa nchini.
kwa upande mwingine baadhi ya wasanii wametoa maoni yao kwa serikali ikiwemo kutumia wasanii kwa lengo la kutangaza vivutio vya Taifa ili kuongeza thamani ya hifadhi za Taifa ambazo zimekuwa msingi waongezeko la fedhazakigeni.
Akihitimisha mjadala huo waziri wa maliasiri na utalii mh Pindi Chana amesema maoni yote ya wadau yaliyo tolewa yatafanyiwa kazi ili kufikialengo la serikali kwa kuongeza pato la taifa kupitia utalii.