

8 April 2025, 6:18 pm
Lengo la kilele cha maadhimisho ya wiki ya afya ni kuimarisha uelewa wa afya, kuangazia maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya afya, na kujadli changamoto zinazoikabili sekta hiyo. Na kauli mbiu ya mwaka huu ni “ Tulipotoka, Tulipo na Tunapolekea Tunajenga Taifa Imara Lenye Afya.”
Na Yussuph Hassan.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, amesema kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Afya Kitaifa 2025 inaakisi mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika sekta ya afya nchini.
Ameyabainisha hayo leo Jijini Dodoma Dodoma katika kilele cha maadhimisho hayo, Dkt. amesema tangu kuanza kwa wiki hiyo shughuli mbalimbali zimefanyika .
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange, amebainisha mafanikio yaliopatikana katika kipindi cha miaka minne ya seriakali ya awamu ya sita katika sekta ya afya.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoama Mhe, Rosemary Senyamule amewapongeza watumishi wa sekta ya afya wanaojitoa kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.