

7 April 2025, 5:42 pm
Zoezi hilo ni enedelevu katika kata hiyo ambapo kila Jumamosi wananchi hujitokeza kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo.
Na Lilian Leopord.
Wananchi wa kata ya Chamwino jijini Dodoma wameshiriki katika zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo.
Akizungumza Diwani wa kata ya Chamwino, Jumanne Ndege katika zoezi hilo, amewapongeza wananchi wa kata hiyo kwa kujitokeza kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo makaburi yaliyopo mkabala na shule ya Sekondari Hijra, lengo ikiwa ni kutekeleza ajenda ya kutunza na kulinda mazingira.
Aidha Diwani Ngede amewataka viongozi wa mitaa kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wate waliokaidi zoezi la kufanya usafi katika kata hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vikundi vya Usafi jiji la Dodoma amewataka wananchi kuzingatia suala la usafi hasa katika maeneo yanayowazunguka. Vilevile ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatunza taka vizuri na wanalipa hela kwa ajili ya taka hizo.
Baadhi ya wananchi walioshiriki katika zoezi hilo akiwemo Amina Mgaya, Balozi wa Chinangali, Shina namba 2 na Mwanaasha Mohamed ambaye ni Mtendaji wa Mtaa wa Mwaja wameelezea jinsi wanavyoshiriki katika kuhakikisha kuwa wanaimarisha usafi wa mazingira.