

2 April 2025, 5:26 pm
Aidha Taswira ya Habari inaendelea na juhudi ya kuutafuta uongozi wa RUWASA wilaya kujua hatua wanazochukua kutatua changamoto hiyo.
Na Victor Chigwada.
Uharibifu wa Miundombinu ya Maji katika kijiji cha Muungano kata ya Muungano umesababisha wananchi kukosa maji hali inayochangia wananchi kutumia muda mrefu kutafuta huduma hiyo.
Baadhi ya wananchi wakizungumza na Taswira ya Habari wamesema zipo juhudi ambazo zimekuwa zimekuwa zikifanyika za kuwa na mafundi lakini bado hawatoshi kupambana na changamoto hiyo ya kupasuka kwa mabomba ya maji
Aidha wamesema hali hiyo imekuwa ikirudisha nyuma juhudi za wakala wa usambazaji maji Vijijini RUWASA .
Wameiomba Mamlaka hiyo kuona namna ya kutandaza mtandao wa bomba zenye ukubwa zaidi ili kukabiliana na changamoto ya kupasuka kwa mabomba mara kwa mara.
Aidha wameiomba Serikali kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto hiyo kwani wananchi wanatumia gharama kubwa kupata maji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Muungano Matonya Mtukamsihi amekiri uwepo wa tatizo Hilo la kupasukaji mabomba na kuiomba mamlaka ya usimamizi wa maji vijijini kuwa karibu na wananchi katika kutoa huduma.