

1 April 2025, 6:09 pm
Ripoti ya takwimu za uhalifu na usalama barabarani ya mwaka 2023 inaonesha matukio ya ubakaji na ulawiti kuongoza ambapo jumla ya matukio 8,185 ya ubakaji yaliripotiwa kwa mwaka 2023 huku ulawiti yakiwa matukio 2,382.
Na Mariam Matundu.
Wakati serikali na wadau mbalimbali wakiendelea na mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili Wilaya za Kondoa na Chemba zimetajwa kuongoza katika matukio ya ulawiti na ubakaji mkoani Dodoma.
Hayo yamebainika kupitia program ya utoaji elimu kuhusu haki za binadamu inayoendeshwa na tume ya haki za binadamu na utawala bora katika wilaya zote za mkoa wa Dodoma .
Florence Chaki ni mkurugenzi wa jinsia kutoa tume hiyo amesema kuwa wamegundua sababu kubwa inayochangia kutokea kwa matukio hayo ni ulevi wa kupindukia.
Amesema pamoja na vyombo vya haki kuhamasisha matukio hayo kuripotiwa lakini bado tabia ya kuyamaliza kifamilia inarudisha nyuma harakati hizo.
Baadhi ya wananchi wa jiji la Dodoma wanatoa maoni yao kuhusu matukio ya ukatili.