

20 March 2025, 5:50 pm
Kampuni ya Puma Energy imetoa mitungi 500 kwa Mheshimiwa mbunge ikielezwa kuwanufaisha mama na baba lishe kutoka vitongoji mbalimbali na vituo vya afya zahanati 51 Dodoma mjini.
Na annwary shaban.
Waziri wa madini na mbunge wa Dodoma mjini Mh.Antony Mavunde ameendelea kuimiza jamii kuzingatia matumizi ya nishati safi ya kupikia katika juhudi za kulinda mazingira na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia suluh Hassan.
Wito huo umetolewa katika Zoez la uzinduzi rasmi wa upatikanaji wa puma energy Tanzania jijini Dodoma Na ugawaji wa mitungi 500 ya gesi kwa babalishe na mamalishe Pamoja na vituo vya afya / zahanati 51 Dodoma mjini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Bi.Fatma M.Abdallah amesema ujio huu wa Puma Gas hautaishia hapa kwani wamejipanga vilivyo kufikia katika kila kona hadi vijijini.
Naye mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri alikuwa na haya ya kusema.