Dodoma FM

Maafisa elimu kata watakiwa kujipambanua

19 March 2025, 5:41 pm

Katibu tawala Mkoa wa Dodoma, Ndugu Kaspar K. Mmuya wakati akifungua mafunzo ya Maafisa Elimu Kata.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Naye Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mwalimu Vicent B. Kayombo amewaasa Maafisa hao kufanya kazi zao kwa bidii , akisisitiza kuwa baada ya mafunzo hayo, wote waliokuwa hawafanyi kazi vizuri wakajirekebishe.

Na Mariam Kasawa.
Maafisa elimu kata watakiwa kujipambanua kwa kuongeza ufaulu na ubora wa elimu.
Hayo yamebainishwa na Katibu tawala Mkoa wa Dodoma, Ndugu Kaspar K. Mmuya wakati akifungua mafunzo ya Maafisa Elimu Kata, yalioandaliwa na Mradi wa Shule Bora chini ya ufadhili wa UK – Aid na kufanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi, Wilayani Kondoa.

Katibu Tawala amewaeleza Maafisa hao kuwa wao ndio wenye jukumu la kusimamia elimu katika kata zao, kwa kuzingatia hilo watimize majukumu yao, kwa kuwa wana dhima kubwa ya kuhakikisha Mkoa unafikisha 95% ya ufaulu kama yalivyo maelekezo ya Mkuu wa Mkoa ,Mheshimiwa Rosemary Senyamule.

Katibu Tawala ametoa Rai kwa Maafisa hao kuishi kimkakati kwa kununua Ardhi- katika Jiji la Dodoma kwani Ardhi inaongezeka thamani, hivyo itawasaidia watakapokuwa wamestaafu.

Sauti ya Katibu Tawala.

Kadhalika amewahimiza juu ya upendo,ambapo amesema kuwa muda wao mwingi wanautumia kazini hivyo ni vema wakawa na upendo na ushirikiano baina yao ili waweze kuishi vizuri, lakini pia wasimamie maslahi ya walimu na wanafunzi katika kata zao ili walimu na wanafunzi hao wawe na furaha. Kwa kufanya hivyo ufundishaji na ujifunzaji utakuwa wenye matokeo.