

13 March 2025, 4:31 pm
Ulaji holela na mtindo wa maisha unatajwa kupelekea wananchi kuugua magonjwa yasio ya kuambukiza.
Na Mariam Kasawa.
Wananchi wametakiwa kuendelea kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama kisukari kwa kubadili mtindo wa maisha.
Katika kuadhimisha miaka 10 ya utoaji huduma Kituo cha Afya Amani na NISUDA March 12 kimewafikia wananchi wa kata ya mpunguzi jijini Dodoma kutoa elimu ya afya juu ya Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza pamoja na upimaji wa magonjwa mbalimbali.
Akizungumza Mganga Mkuu wa Kituo Cha afya Amani Dkt Kamugisha Dominick kilichopo Area D Jijini Dodoma kwa kushirikiana na NISUDA iliyopo kisasa anasema wanaendelea kuhamasisha wananchi kupima afya zao.
Denis Kamagi ni Meneja wa huduma kutoka kituo cha afya Amani Pamoja na NISUDA anasema Moja ya Changamoto kubwa kwa wananchi wengi ni kuwa na uzito mkubwa tofauti na wanavyopaswa kuwa kutokana na mtindo wa maisha ikiwemo ulaji holela.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi walio jitokeza katika eneo hilo kupima afya zao walikuwa na haya ya kusema.