Dodoma FM

Tunawezaje kuondoa ukatili wa kiuchumi kwenye familia?

5 March 2025, 1:14 pm

Ukatili wa kiuchumi kitendo cha kikatili ambacho mtu mmoja anaweza kumiliki kwa nguvu vyanzo vya uchumi vya mtu mwingine.Picha na google.

Katika kufahamu suala hilo mwandishi wetu Alfred Bulahya amefanya mahojiano na mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya GFF.

Na Alfred Bulahya.
Tunapozungumzia ukatili wa kiuchumi ni kitendo cha kikatili ambacho mtu mmoja anaweza kumiliki kwa nguvu vyanzo vya uchumi vya mtu mwingine.

Aidha ni vitendo vya kumnyima mtu fursa ya kupata mahitaji ya msingi na ya kujiendeleza kama kumkataza mke/mume kufanya kazi, kuzuia fedha za matumizi na kumtolea maneno ya masimango, kejeli wakati wa kumpatia fedha kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kifamilia au binafsi; mfano ununuzi wa mahitaji ya nyumbani, nguo, matibabu, kumnyima mke kushika au kumiliki fedha, kutumia fedha/mali za familia bila ridhaa ya mwingine mathalan kuendesha gari la familia, kumnyima kumiliki mali na vitendo vingine vinavyosababisha msongo wa mawazo.