Dodoma FM

Msangalale walia na SGR kuharibu makazi yao

5 March 2025, 12:13 pm

Picha ni wakazi wa Msangalalee wakitoa malalamiko yao kwa mkuu wa wilaya ya Dodoma. Picha na Jambo Tv.

Wakazi wa maeneo hayo wamesema wamekuwa wakilalamika tangu mwaka 2019.

Na Anwary Shaban.
Wanachi Dodoma walia uwepo wa SGR unavyoharibu makazi yao.

Wananchi wa kitongoji cha Msangalale kata ya Makulu jijini Dodoma wamelalamikia uharibifu wanaoupata kutokana na mafuriko ya maji yanayotoka vyanzo vingine na kuathiri makazi yao kupitia mkondo wa maji uliojengwa wakati wa ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa SGR.

Wakizungumza wananchi hao jijini humo wamesema kuwa mbali na tatizo la mikondo ya maji pia barabara walizokuwa wakizitumia zimezibwa hali inayowafanya kushindwa kupitisha magari, hali hiyo imeathiri upatikanaji wa huduma za dharura .

Mbali na tatizo la mikondo ya maji pia Barabara walizokuwa wakizitumia zimezibwa .Picha na jambo Tv.
Sauti za wananchi.

Aidha wakazi wa maeneo hayo wamesema wamekuwa wakilalamika tangu mwaka 2019, lakini bado hawajapatiwa suluhisho.

Baada ya kusikiliza kero za wananchi wa maeneo hayo mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini na mkurugenzi wa Halmshauri ya jiji la Dodoma nae alikuwa na haya ya kusema.

Sauti ya Mkurugenzi