Dodoma FM

JKCI yasema takriban wagonjwa 2,784 wafanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo

27 February 2025, 1:26 pm

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge, ameeleza mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo.Picha Alfed Bulahya.

Amesema katika wagonjwa hao watu wazima walikuwa 1,880 na watoto 904.

Na Alfred Bulahya.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI imefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa wagonjwa 2,784 wakifanyiwa upasuaji wa mishipa ya damu na mapafu.

Hayo yameelezwa Februari, 26, 2025 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.

Amesema katika wagonjwa hao watu wazima walikuwa 1,880 na watoto 904.

Sauti ya Dkt. Peter Kisenge.

Katika kuboresha huduma za afya nchini, JKCI imefunga mtambo wa kuzalisha hewa ya oksigeni wenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 utakaotumika kusambaza hewa ya oksijeni kwa wagonjwa wenye uhitaji na kupunguza gharama za kununua mitungi ya oksijeni kama ilivyokuwa awali.

katika wagonjwa hao watu wazima walikuwa 1,880 na watoto 904.Picha na Alfred Bulahya.
Sauti ya Dkt. Peter Kisenge.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ni Hospitali maalum na Chuo Kikuu cha mafunzo ya utaalamu wa matibabu ya moyo inayomilikiwa na Serikali inayotoa mafunzo na huduma za utafiti wa moyo.