Dodoma FM

TEA yatenga shilingi bilioni 3.0 kuimarisha miundombinu mafunzo ya amali

27 February 2025, 1:07 pm

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dkt.Erasmus Kipesha wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TEA kwa miaka 4.Picha na Alfred Bulahya.

Shule 20 zitanufaika na mpango huo zikiwemo shule za Sekondari zinazotoa mafunzo ya ubunifu na ufundi stadi.

Na Alfred Bulahya.
Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) imetenga fedha kiasi cha bilioni 3.0 kwajili ya kuimarisha miundombinu ya utoaji wa mafunzo ya amali ili kufanikisha utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dkt.Erasmus Kipesha wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TEA kwa miaka 4 ya serikali ya awamu ya 6.

Amesema shule 20 zitanufaika na mpango huo zikiwemo shule za Sekondari zinazotoa mafunzo ya ubunifu na ufundi stadi.

Shilingi bilioni 3.0 zitatumika kuboresha miundombinu ya shule kwaajili ya mtaala mpya.Picha na Alfred Bulahya.
Sauti ya Dkt.Erasmus Kipesha.

Aidha Dkt.Kipesha amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/25 TEA imepanga kufadhili jumla ya miradi 113 ya kuboresha miundombinu ya elimu katika shule za msingi na Sekondari kwenye maeneo mbalimbali nchini yenye thamani ya sh.bil.11.3.

Aidha ametoa wito kwa WADAU mbalimbali nchini kuendelea kuiunga mkono Serikali kwa kuchangia sekta ya elimu kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa ili kuiendeleza sekta hiyo.

Sauti ya Dkt.Erasmus Kipesha.