

25 February 2025, 6:18 pm
Magonjwa ya moyo kwa watoto yanaweza kuchangiwa na NCDs, na maambukizi kwa wazazi au mtoto.
Imeelezwa kuwa utambuzi mdogo kwa jamii juu ya magonjwa ya moyo kwa watoto, imetajwa kuwa sababu ya watoto wanaosumbuliwa na magonjwa hayo kuchelewa kupata matibabu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Prof Abel Makubi, wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kambi ya pamoja ya matibabu ya moyo kwa watoto inayotekelezwa na BMH na madaktari bingwa wa moyo kutoka Shirika la Children Heart Association la Kuwait.
Aidha amewataka wazazi na walezi wenye watoto wenye matatizo ya moyo wameombwa kuwaleta kwenye kambi ya matibabu ya moyo ya ushirikiano wa mabingwa wa Benjamin Mkapa Hospital na Kuwait kwa watoto iliyoanza tarehe 21 mpaka 28 Februari .
Prof Makubi ametaja dalili za matatizo ya moyo kwa watoto kuwa ni kupumua kwa shida, kikohozi cha mara kwa mara, mtoto kushindwa kunyonya na kutokwa na jasho jingi na kutoongezeka uzito.
Kwa upande wake, kiongozi wa msafara wa timu ya wataalamu kutoka Kuwait, Prof. Faisal Al-Saidei, amesema lengo la wao kushirikiana na BMH ni kutoa matibabu ya moyo kwa watoto waliozaliwa na matatizo ya moyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tiba wa BMH, Dkt. Kessy Shija, magonjwa ya moyo kwa watoto yanaweza kuchangiwa na NCDs, na maambukizi kwa wazazi au mtoto.
.