

20 February 2025, 7:45 pm
Na Alfred Bulahya.
Wazazi katika kata ya Mbabala jijini Dodoma wametakiwa kuhakikisha wanazingatia kutoa mahitaji yote ya msingi kwa watoto wao ili kuepusha tatizo la kukatisha masomo.
Wito huo umetolewa na Afisa elimu Kata ya Mbabala Mwalimu Shaban Kijoji wakati akizungumza na taswira ya habari.
Mwl Kijoji amezitaja faida zinazopatikana endapo wavulana na wasichana hawatakatisha masomo yao.