

19 February 2025, 6:22 pm
Mwandishi wetu Selemani Kodima ametuandalia taarifa ifuatayo kuhusu mwanamke aliyesoma sayansi.
Na Mwandishi wetu.
Itakumbukwa hivi karibuni Dunia iliadhimisha siku ya wanawake na wasichana katika Sayansi.
Kwa mujibu wa takwimu za elimu na ajira duniani zinaonesha kuwa ushiriki wa wanawake na wasichana katika elimu na ajira katika fani za sayansi ni mdogo ikilinganishwa na ushiriki wa wanaume hali ambayo inapunguza juhudi za kufikia usawa wa kijinsia katika elimu na ajira.