

19 February 2025, 3:46 pm
Amewataka Makatibu wa Matawi wa Chama hicho kutenda haki, kutopuuza Katiba na kujiepusha na masuala ya RUSHWA.
Na Seleman Kodima.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emanuel Nchimbi amewataka Makatibu wa Matawi wa Chama hicho kutenda haki, kutopuuza Katiba na kujiepusha na masuala ya RUSHWA wakati Chama kikielekea kwenye uchaguzi Mkuu 2025.
Balozi Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Februari 19,2025 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa Watendaji wa Kata na Makatibu Tawi wa Chama hicho kwa Mkoa wa Dodoma.