Dodoma FM

Sekta ya michezo yapiga hatua

18 February 2025, 7:17 pm

Picha ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma.Picha na Alfred Bulahya.

Katika hatua Nyingine ameitaja mikakati ya serikali iliyopo katika kuendelea kuikuza sekta ya michezo nchini.

Na Alfred Bulahya.
Kufuatia Serikali Nchini kuiongezea Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bajeti ya fedha kutoka shilingi bilioni 35.44 mwaka 2021/2022 hadi shilingi bilioni 258 mwaka wa fedha 2024/2025, sekta ya michezo imepiga hatua kubwa ikiwa ni ishara ya kukua kwa uchumi wa nchi.

Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya baraza hilo kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema Katika mafanikio hayo upo ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya michezo, kwenye viwanja mbalimbali ikiwemo uwanja wa Benjamin Mkapa, na ujenzi wa uwanja mpya wa Dodoma.

Sauti ya Bi. Neema Msitha.

Ametaja mafanikio mengine kuwa ni Tanzania kuwa mwenyeji wa matukio makubwa ya michezo ya Kimataifa, kuondoa kodi kwa nyasi bandia, Tanzania kuwa Makao Makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Afrika Kanda ya Tano na kuanzishwa kwa Mfuko wa Michezo.

Picha ni aina ya kiwanja cha michezo ambacho kinatarajiwa kujengwa.Picha na Alfred Bulahya.
Sauti ya Bi. Neema Msitha.

Katika hatua Nyingine ameitaja mikakati ya serikali iliyopo katika kuendelea kuikuza sekta ya michezo nchini.

Sauti ya Bi. Neema Msitha.