

11 February 2025, 5:14 pm
Rasimu hii ya Bajeti imepitishwa kutumika Elfu Mbili na ishirini na Tano (2025) ishirini na Sita(2026).
Na Kitana Hamis.
Wananchi wilayani Kiteto wameishauri Bajeti ya zaidi ya shilingi billioni 38 iliyopitishwa na Baraza la madiwani itatue changamoto zinazo wakabili katika sekta ya Afya na elimu.
Rasimu hii ya Bajeti imepitishwa kutumika Elfu Mbili na ishirini na Tano (2025) ishirini na Sita(2026) Baadhi ya Wananchi wakawa na yakusema Juu ya Bajeti hiyo.
Dodoma Tv tumezungumza na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Abdala Mbundala kujua tafsiri halisi ya Bajeti hii kwa Wananchi kulingana na Hali ilivyo kwa sasa ambapo amesema Bajeti iiliyopitishwa ni katika ile Miradi ya Maendeleo au zile kazi za Maendeleo zinazofanyika Moja kwa Moja kwa Wananchi.
Afisa Mipango wa Wilayani Kiteto ametaja Vipao Mbele Juu ya Bajeti amesema upatikanaji wa Sekta ya Afya upande wa madawa na Vifaa sehemu zote za Zahanati Vituo vya Afya Pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Kiteto Pamoja na ununuzi vifaa vya Kisasa vitakuwa Kwenye Vituo hivyo ya kutolea Huduma vilevile Wananchi Sekta watakayo guswa zaidi ni Elimu kuazia Shule ya Msingi na Secondari .
Kwaupande Madiwani wakati wanapitisha Bajeti hii wakawa na machache yakusema.