Dodoma FM

Akutwa amejinyonga kwenye kingo za mto

7 February 2025, 5:17 pm

Picha ni wakazi wamtaa wa Maisaka B Mjini Babati Mkoani Manyara wakiwa katika kingo za mto huo.Picha na Kitana Hamis.

Wananchi wa Eneo hilo walipata wasaa wa Kuzungumza na Dodoma Tv Juu ya Tukio hilo.

Na Kitana Hamis.
Mwanamke Mmoja ambaye Hajafahamika jina lake anadaiwa kujinyonga hadi kufarikia dunia Wilayani Babati Mkoani Manyara.

Nitukio la kutatanisha ambapo limetoke katika mtaa wa Maisaka B Mjini Babati Mkoani Manyara ambapo Mwili wa mwanamke huyo Umekutwa Kwenye kingo ya Mto bila nguo hata hivyo chazo cha Tukio hilo bado hakijajulikana .

Wananchi wa Eneo hilo walipata wasaa wa Kuzungumza na Dodoma Tv Juu ya Tukio hilo pamoja na mambo mengine Waliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kwa kina juu ya Tukio hili.