Dodoma FM

‘Wanaume washirikishwe mapambano dhidi ya ukatili’

6 February 2025, 4:58 pm

Picha ni baadhi ya wanaume wilani Kiteto wakiwa katika mkutano huo.Picha na Kitana Hamis.

Wanaume wangeshirikishwa kikamilifu kupinga vitendo vya ukatili ikiwemo ukeketaji vigeisha.”

Na Kitana Hamis.
Wananchi wilayani Kiteto wameitaka serikali kuwashirikisha wanaume zaidi katika mapambano ya vitendo vya ukatili ili yaweze kupungua.

Wakizungumza na Dodoma Tv baadhi ya wananchi wilayani Kiteto mkoani Manyara wamesema wanaume wangeshirikishwa kikamilifu kupinga vitendo vya ukatili ikiwemo ukeketaji vingeisha.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kaloleni wilayani Kiteto mkoani Manyara Shabani sindalo amezungumzia Ukatili Katika eneo lake na nakueleza juhudi za serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili.

Picha ni mkazi wa wilaya ya Kiteto akizungumza na mwandishi wetu juu ya vindo vya ukatili. Picha na Kitana Hamis.

Amesema vitendo vya ukeketaji pamoja na ukatili wa vipigo upo lakini serikali inaendelea kuelimisha wananchi na jamii kiujumla juu ya ukatili huu na wananchi wanaonesha kuelewa siku hadi siku.

Katika kuisaidia Serikali kukabiliana na Vitedo vya Kikatili ikiwemo Ukeketaji, Vipingo, Ulawiti wadau wa Maendeleo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara wameeleza namna watakavyowafikia wananchi elfu thelathini (30) na kutoa elimu juu ya vitendo hivyo.