Dodoma FM

Bodi ya wakurugenzi UCSAF yasisitizwa kukamilisha ujenzi wa minara 758

5 February 2025, 12:24 pm

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa , akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) .Picha na Mariam Matundu.

Waziri Slaa ameitaka bodi kuzingatia miongozo, taratibu na sheria za uendeshaji wa shughuli za Bodi, ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu yao unakuwa wa ufanisi na wenye tija.

Na Mariam Matundu.
Waziri wa mawasiliano na teknolojia ya habari Mhe Jerry Sillaa ameitaka bodi ya wakurugenzi mfuko wa mawasiliano kwa wote kuhakikisha inatekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwemo kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa minara 758.

Akizungumza wakati akizindua bodi hiyo waziri Silaa amesema bodi hiyo inawajibu mkubwa katika kuhakikisha mkakati wa kuimarisha uchumi wa kidijitari ambapo ujenzi wa minara hiyo ni nguzo muhimu.
Amesema mpaka mwezi Januari mwaka 2025 tayari minara 380 imekwisha kuwashwa na kwamba minara iliyobakia inapaswa kuwashwa hadi kufikia mwezi mei mwaka 2025.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed K. Abdulla akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) 
Sauti ya Mhe. Jerry Silaa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF Balozi Valentino Longino Mlowola amesema watahakikisha wanawashirikisha wadau wote wanaohusika ili kuweza kukamlisha minara hiyo kwa wakati ambapo wanatarajia kukamilisha kwa wakati.

Sauti ya Balozi Valentino Longino Mlowola

Kukamilika kwa ujenzi wa kinara 758 hapa nchini kutawezesha taifa kupiga hatua Zaidi katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitari.