

3 February 2025, 12:58 pm
Kukithiri kwa Vitendo hivi kumeibua ofisi ya Mashitaka nchini Dpp kuazisha Ofisi ndogo Kiteto.
Na Kitana Hamis.
Suala la ukatili wa kijinsia limeshika kasi katika wilaya ya Kiteto ambapo kwa mujibu wa wenyeji wa wilaya hii wanalalamika kuwa vitendo vya ukatili wa kingono ikiwemo ulawiti na ubakaji vimekithiri sana katika eneo hili.
Makudi yanayoadhirika sana ndani ya Jamii kutokana na ukatili huu nipamoja na Watoto wadogo ambao wao hata kujitetea wenyewe hawawezi .
Kukithiri kwa Vitendo hivi kumeibua ofisi ya Mashitaka nchini Dpp kuazisha Ofisi ndogo Kiteto ili kurahisisha usikilizaji wa kesi hizo .
Akizungumza na Dodoma tv katika wiki ya Sheria ambapo kilele chake ni leo feb 3/2025 Eliakimu Msengi amesema dawati la polisi wilayani Kiteto linapaswa kuendelea kushirikiana na wananchi kupambana na ukatili huu ambao umekithiri wiwlwyani humo.
Raisi wa jumhuri ya Mungano wa Tanzania Daktari Samia Suluh Hasan ameanzisha Kampeni ya msaada wa Kisheria legal eid campaign kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ambapo Afisa wa Maendeleo ya Jamii Kiteto anasema sambamba na wananchi kujua Haki zao pia wanapaswa wajue niwapi Mahali pakupeleka ili waweze Kusaidiwa .
Hakimu wa Mahakama ya mwanzo Kibaya Msuya akiwa na timu ya watoa msaada wa kisheria shule ya msingi boma mbele ya wanafunzi pamoja na walimu wao amesema wanapaswa kufahamu mambo mbalimbali yanayo husu sheria.