Wajawazito Muungano wachangia chumba kimoja na wagonjwa wa kawaida
27 January 2025, 3:45 pm
Jengo la mama na mtoto mpaka sasa limefikia hatua ya renta ambapo kwa sasa ujenzi umesimama kutokana na kuishiwa fedha za kuendeleza.
Na Seleman Kodima.
Uchache wa majengo katika zahanati ya Muungano umesababisha akina mama wajawazito kutumia chumba kimoja kujifungulia.
Wakizungumza na Taswira ya Habari baadhi ya wananchi wamesema kuwa kitendo cha akina mama wajawazito kuchangia chumba kimoja na mgonjwa wa kawaida imekuwa ni fedheha na aibu kwao.
Aidha wameiomba serikali kufanya maboresho katika zahanati hiyo ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa jengo la mama na mtoto.
Matonya Mtukamsihi ni mweyekiti wa kijiji cha Muungano amesema kutokana na uhitaji wa wananchi zipo hatua ambazo zimechukuliwa kwaajili kukabiliana na changamoto hiyo.
Mtukamsihi ameongeza kuwa kukamilika Kwa ujenzi wa huo itaondoa fedheha wanayoipata wananchi.
Jengo la mama na mtoto mpaka Sasa limefikia hatua ya lenta ambapo kwasasa ujenzi umesimama kutokana na kuishiwa fedha za kuendeleza ambapo kukamilika kwake kunatarajiwa kuwa tumaini jipya Kwa Wanamuungano