

16 January 2025, 3:23 pm
Dodoma FM imezungumza na mama wa mtoto ambaye anadai kuwa hawezi kumsomesha mtoto huyo.
Na Kitana Hamis.
Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, ameieleza Dodoma FM kuwa mama yake tayari alipokea mahari ili kumwozesha binti huyo ambapo binti huyo aliamua kuomba msaada kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Kiteto.
Dodoma FM imezungumza na mama wa mtoto ambaye anadai kuwa hawezi kumsomesha mtoto huyo kutokana na maisha kuwa magumu kutokana na mume wake kufariki na kumwachia watoto 9 ambao anawajibika kuwatunza mwenyewe huku akikiri kuwa anashindwa kumudu kuwasomesha watoto hao kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu.
Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma Takukuru naye anaeleza namna alivyompokea mtoto huyo .
Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Kiteto anasema tayari wamewasiliana na uongozi wa shule ya sekondari aliyopangiwa ambapo wameridhia huyo mtoto aanze shule mara moja.