Dodoma FM

Tunawezaje kudhibiti ukatili wa kijinsia mahala pa kazi

15 January 2025, 5:09 pm

Unyanyasaji kijinsia mahali pa kazi ni ubaguzi na umekatazwa kisheria na ni sehemu ya Kanuni za adhabu.Picha na TGNP.

Mwandishi wetu Alfred Bulahya ametuandalia kisa kuhusu Shujaa aliyemsaidia muhanga wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia mahala pa kazi.

Na Seleman Kodima.
Umoja wa Mataifa, unafafanua kuwa Ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote anachofanyiwa mtu yeyote awe mwanamke, mwanaume au mtoto, kinacholenga kumuumiza kimwili au kiutu.

Ingawa ukatili wa kijinsia anaweza kufanyiwa mtu yeyote, kundi la wanawake na watoto ndio wahanga wakubwa wa ukatili wa kijinsia.

Kwa Mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini 2004; Sura ya 138 (D) ya kanuni za adhabu, 1945
Anayekutwa na hatia ya kufanya hivyo, ataweza kupata kifungo cha hadi miaka mitano, au faini isiyozidi shilingi laki mbili au vyote kwa pamoja, na pia anaweza kupewa amrisho la kulipa fidia kwa aliyeathirika kama itakavyo amriwa na mahakama.

Matendo ya ngono yatakayo sababishwa kwa maneno au matendo na mtu aliye na madaraka katika sehemu ya kazi au sehemu nyingine yoyote, atakuwa ametenda kosa la udhalilishaji wa kijinsia.