Wazazi na walezi watakiwa kutimiza wajibu kwa watoto wao
15 January 2025, 4:45 pm
Ajenda ya maendeleo ambayo inalenga kuhakikisha kwamba “hakuna anaebaki nyuma,”ikiwa ni pamoja na ahadi ya kuhakikisha elimu jumuishi na bora kwa wote.
Na Seleman Kodima.
Imeelezwa kuwa ili kuvishinda vikwazo vinavyomkwamisha mtoto wa kike kusoma na kutimiza malengo yake ni wazazi na walezi kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha wanatimizia mahitaji yote watoto wao.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti Baadhi ya wazazi na walezi wametaja baadhi ya Vikwazo vinavyokwamisha msichana kupata elimu na hitamaye kutimiza malengo yake.
Shukrani Mbarani ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Mpunguzi amesema baadhi ya Vikwazo vinasababisha na ushirikiano mdogo baina ya mzazi na mwalimu.
Kwa upande mwingine Mwl Mbarani amesema kitendo cha Mwanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule inaweza kusababisha athari mbalimbali kwa msichana.
Jitahada za kuondoa Vikwazo hivi ni kuhakikisa Tanzania inatimiza na kutekeleza moja ya maazimio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs).