Wananchi Ihumwa wapewa tahadhari mlipuko wa kipindupindu
13 January 2025, 4:39 pm
Picha ni vimelea vya Kipindipindu .Picha na Google.
Hayo yameelezwa na Katibu Kata wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg.Lazaro Chiswagala alipo kuwa akiongea na waumini wa kanisa la MT.Joseph Ihumwa
Na Victor Chigwada .
Wananchi wa mtaa wa Ihumwa A wapewa tahadhari ya kukabiliana na ugonjwa wa mlipuko wa matumbo ya kuhara alimaarufu ugonjwa kipindupindu.
Hayo yameelezwa na Katibu Kata wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg.Lazaro Chiswagala alipo kuwa akiongea na waumini wa kanisa la MT.Joseph Ihumwa.
Amewataka watu kuaacha kuzoea ugonjwa na baadala yake waonapo dalili za kuugua tumbo ni vyema kufika zahanati au kituo cha afya kupata ushauri au tiba.
Chiswagala amewata waumini hao kufuata kanuni za usafi katika kukabiliana na hatari ya ugonjwa huo
Huku akiwasisitiza kuacha tabia ya kujificha pindi wanapo ugua kwa kuhofia kufika zahanati au kituo cha afya.
Aidha Chiswagal amewataka wananchi wa Ihumwa kuitumia zahanati yao kwa manufa yao kwani zipo huduma za kujitosheleza badala ya kukimbilia vituo binafsi.
Kwani kufanya hivyo inapunguza maaana ya maboresho yaliyo fanyika ya kuongeza upatikanaji wa huduma kwa jamii ikiwa ni p[amoja na matibabu ya dharula.