Dodoma FM

Kidoka waomba serikali kuingilia kati ujenzi wa sekondari

2 January 2025, 5:56 pm

Picha ni wakazi wa kijiji cha Kidoka wakiwa katika mkutano wa Kijiji. Picha na Nizar Mafita.

Wakazi wa kijiji hicho wameendelea kuiomba serikali kuingilia kati suala hilo la ujenzi wa sekondari kijijini hapo kwani ni la muda mrefu.

Na Mariam Kasawa.
Wakazi wa Kijiji cha Pangalua kata ya Kidoka wilayani Chemba walalamikia ucheleweshaji wa ujenzi wa Sekondari ya kata ambayo ilitakiwa kujengwa katika eneo hilo.

Wakiongea katika mkutano wa kijiji ulio wakutanisha wakazi wa eneo hilo na viongozi wa kata wananchi hao wamedai kuhujumiwa katika ujenzi huo wa sekondari kutokana na viongozi kuhamisha mradi huo wa ujenzi na kuupeleka katika kijiji cha Kidoka.

Sauti za wananchi.
Picha ni Katibu wa ccm kata ya Kidoka Bw Mohamed Masare akiongea katika mkutano huo.Picha na Nizar Mafita.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kidoka Bw. Baraka Lemoyan anasema licha ya Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya kutoa kauli ya ujenzi wa sekondari kayika eneo hilo lakini hadi leo ujenzi huo haujatekelezwa hali inayo leta sintofahamu kwa wananchi.

Sauti ya Bw. Baraka Lemoyan.

Katibu wa ccm kata ya Kidoka Bw Mohamed Masare ameiomba serikali kuunda tume ili ikafanye uchunguzi juu ya kukwama kwa ujenzi wa Sekondari hiyo.

Sauti ya Bw Mohamed Masare.