Dodoma FM

Wananchi Nala, Chihoni wapatiwa elimu ya kupinga ukatili

23 December 2024, 5:36 pm

Picha ni Afisa maendeleo ya Jamii Kata ya Chamwino, Cecilia Oswago akiongea na wananchi hao.Picha na Annuary Shaban.

Wazazi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwalea watoto wao kwa kutenga muda wa kuzungumza nao na kuwajengea uwezo wa kuzungumza kipindi wakipata matatizo.

Na Annuary Shaban.
Wakazi wa Mtaa wa Nala, Segu Juu, Segu Chini na Chihoni, wamewezeshwa elimu ya kupinga Ukatili wa kijinsia, Malezi na Makuzi, Uchumi na Afya ya uzazi katika Kata ya Nala Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu ya Malezi na Makuzi, Afisa maendeleo ya Jamii Kata ya Chamwino, Cecilia Oswago, ambaye alimuwakilisha Mratibu wa Dawati la Jinsia Idara ya Maendeleo ya Jamii Fatuma Kitojo.

Amesema kuwa wazazi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwalea watoto wao kwa kutenga muda wa kuzungumza nao na kuwajengea uwezo wa kuzungumza kipindi wakipata matatizo kwa kuzingatia haki ya mtoto na wajibu.

Sauti ya Cecilia Oswago.

Naye, Afisa Maendeleo Kata ya Nala, Monica Lugaila, aliwezesha elimu ya ukati na afya uzazi na kuwataka wazazi kuwa mstari wa mbele kupinga ukatili kwa watoto kwa kutowaozesha wakiwa na umri mdogo.