Serikali yaendelea na ukarabati miundombinu ya maji soko la Machinga
6 December 2024, 11:50 am
Soko la machinga lilianza kufanyakazi November 1, 2022, kwa mujibu wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma hadi sasa soko hilo linahudumia wajasiriamali zaidi ya 3200 waliosajiliwa, linatoa huduma mbalimbali zikiwemo huduma za vyakula, biashara za nguo, mapambo, huduma za kibenk .
Na Ramadhan Idd.
Wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex Jijini Dodoma wameombwa kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho Serikali inaendelea na mchakato wa kukarabati maeneo yote ya wazi yanayopitisha maji ndani ya soko na kuathiri shughuli zao.
Hali hiyo inatajwa kuwa kero kwa muda mrefu, ikisababisha hasara kwa wafanyabiashara pamoja na kuzorotesha shughuli za kila siku sokoni hapo.
Miongoni mwa wahanga ambao biashara zinaharibiwa na mvua ni wafanyabishara wa chakula eneo la Block A na hapa wanazungumza.
Athumani Muhanga ni kiongozi na Balozi wa eneo hilo amewataka wafanyabishara hao kuwa watulivu kwani serikali inafahamu changamoto zao.
Naye Mwenyekiti wa Soko la Machinga Nyamageni Kingamkono amebainisha kuwa soko hilo litafanyiwa maboresho katika maeneo yote yenye changamoto na mchakato umefikia hatua nzuri.