Dodoma FM
Wanaume watakiwa kujitokeza kupima VVU
4 December 2024, 11:16 am
Wanaume wametakiwa kuacha tabia ya kusubiri wake zao wapime na kujiona wapo salama baada ya majibu.
Na Lilian Leopord.
Hofu na uoga kwa baadhi ya wanaume imeelezwa kuwa chanzo kikubwa kinachowafanya kushindwa kujitokeza kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Wakizungumza na Dodoma Tv baadhi ya Wakazi mkoani Dodoma wamesema hali hiyo bado imeendelea kuwarudisha nyuma katika kujua hali zao kiafya.
katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa alitoa wito kwa wanaume wote nchini kupima maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ili kujua afya zao na kuacha tabia ya kusubiri wake zao wapime na kujiona wapo salama baada ya majibu.