Serikali kuendeleza ushirikiano na wajariamali wa Zabibu
3 December 2024, 11:43 am
Serikali imeendelea kuwataka wawekezaji wengi kuja kuwekeza katika Mkoa wa Dodoma.
Na Fred Cheti.
Serikali imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wajasirimali wadogo,wakati na wakubwa wa zao la zabibu ili kuzidi kukuza biashara hiyo pamoja uchumi wa nchi kwa ujumla.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya ameyasema hayo wakati akifunga maonesho ya zabibu festival kwa niaba waziri wa ujenzi yalifanyika jijini Dodoma katika viwanja vya zamani vya Mashujaa.
Katika hatua nyingine Mhe Kasekenya amewataka wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza katika Mkoa wa Dodoma kwani kuna uwepo wa fursa nyingi kwa sasa kutokana na ukuaji wake huku akipongeza wadau mbalimbali kwa kuleta teknolojia nyingi zinazosaidia katika sekta ya ujenzi.
Kwa upande wake Mratibu wa Maonesho hayo bwana Mat Builders alikua na haya ya kusema.