Dodoma FM
Mimba za utotoni bado ni tatizo kwa taifa
3 October 2024, 8:10 pm
Na Lilian Leopold
Tatizo la mimba za utotoni limekuwa ni suala endelevu katika jamii nyingi nchini Tanzania.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dodoma kutoka Dawati la Kijinsia Bwn. Michael Nkinda amebainisha sababu mbalilmbali zinazopelekea kuwepo kwa tatizo hilo miongoni mwa jamii wakati akizungumza na Dodoma TV.
Aidha, Bwn, Micheal amebainisha mikakati iliyowekwa ili kukabiliana na mimba za utotoni katika ngazi za kijamii, mkoa na kitaifa.
Nao baadhi ya wazazi wamesema kuwa ni vyema kupunguza majukumu ili kupata muda wa kutosha wa kuzungumza na watoto wao na kuwafundisha maadili mema.