Dodoma FM

Je, vijana wanaelewa kuhusu chanzo cha magojwa ya moyo?

2 October 2024, 8:58 pm

Na Yussuph Hassan.

Imeelezwa kuwa vijana nchini Tanzania wapo katika hatari ya kupata magojwa ya moyo kutokana na mtindo wa maisha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Prof. Abel Makubi  alithibitisha hilo mapema wiki hii  katika mkutano uliowakutanisha waandishi wa habari pamoja na wadau wa afya katika Hospital ya Benjamin Mkapa wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya magojwa ya moyo toka kwa wahisani wa Uholanzi.

Mwandishi wetu amefanya mahojiano na baadhi ya vijana jijini Dodoma kutaka kujua wana uelewa gani juu ya nini kinaweza kuwa chanzo cha magojwa ya moyo ambayo yanatajwa kuathiri kundi kubwa la vijana.

Pichani ni moja ya kijana mkazi wa Dodoma akieleza juu ya uelewa wake kuhusu chanzo cha magonjwa ya moyo kwa vijana.
Sauti za wananchi
Pichani ni moja ya kijana mkazi wa Dodoma akieleza juu ya uelewa wake kuhusu chanzo cha magonjwa ya moyo kwa vijana.