Dodoma FM

Sango Darajani hatarini magonjwa ya mlipuko

13 September 2024, 7:29 pm

Picha kuonesha maji taka yanayotiririka katika mitara Sango Darajani katika soko la Majengo jijini Dodoma

Wafanyabiashara wa vyakula wanasema eneo hilo ni hatari kwa biashara zao kwani inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko.

Na Fatuma Maneno .

Wananchi na wafanyabiashara wa Sango Darajani jijini Dodoma katika soko la Majengo, wamehofia usalama wa afya zao kutokana na uwepo wa maji taka yanayotiririka katika mitaro iliyopo jirani na eneo hilo.

Wamesema maji taka hayo husababisha harufu mbaya katika eneo hilo hali inayopelekea kushindwa kukaa eneo hilo na hivyo wameomba uongozi wa eneo hilo usaidie kufanyika usafi wa mara kwa mara ili kupunguza kadhia hiyo.

Mkazi wa Sango Darajani
Sauti za wakazi Sango Darajani

Aidha, wafanyabiashara wa vyakula wanasema eneo hilo ni hatari kwa biashara zao kwani inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kutokana na harufu mbaya inayoyotokana na maji taka hayo.

Mfanyabiashara Sango Darajani
Sauti za wafanyabiashara
Mfanyabiashara Sango Darajaani

Jitihada za kumtafuta mwenyekiti wa eneo hilo kuzungumzia suala  hili bado zinaendelea.