Dodoma FM

Dhana ya 50/50 si yakushindana na wanaume

28 August 2024, 2:23 pm

Picha ni Mkururugenzi wa wa mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Bi Lilian Liundi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika Tamasha la 7 la jinsia ngazi ya wilaya linalo  fanyika wilayani Kondoa.Picha na Mariam Kasawa.

Imeelezwa kuwa kupitia dhana ya hamsini kwa hamsini ambayo inamjenga mwanamke kushiriki katika kila idara sawa kwa sawa na mwanaume dhana hii imepokelewa tofauti na baadhi ya jamii.

Na Mariam Kasawa.

Wakati serikali ikiwa katika mchakato wa maandalizi ya Dira mpya ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050, Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP umetaka uwakilishi wa wanawake katika ngazi za maamuzi ujumuishwe katika maandalizi ya dira hiyo ili kuongeza uwakilishi huo na kufikia 50/50.

Hayo yamebainishwa na Mkururugenzi wa wa mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Bi Lilian Liundi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika tamasha la 7 la jinsia ngazi ya wilaya linalofanyika wilayani Kondoa ambalo limewakutanisha wadau zaidi ya 200.

Picha ni wanawake wakiwa katika viwanja vya Sabasaba katika tamasha la jinsia ngazi ya wilaya linalo fanyika katika wilayani Kondoa.Picha Mariam Kasawa.

Bi. Liundi amesema katika kwa mujibu wa riport  ya uchaguzi wa serikali za mitaa ya mwaka 2019 bado idadi ya uwakiishi wa wanawake katika ngazi za maamuzi ni ndogo hivyo jitihada zinatakiwa kuendelea kufanyika ili kuongeza uwakilishi huo kufikia 50/50.

Clip……………. liundi

Wakizungumza baadhi ya wanawake wilayani Kondoa wamesema wamewataka wanawake kuielewa dhana hii na si kuitumia tofauti hali inayopelekea wanaume kutumia mabavu.

Clip…………..wanawake