Dodoma FM

Elimu ya matumizi sahihi ya ardhi yawanufaisha vijana

16 August 2024, 11:40 am

Picha ni Darasa la mafunzo ya umiliki ardhi kwa vijana katika ukumbi wa SIDO jijini Dodoma.Picha na George John.

Mitazamo hasi ya baadhi ya vijana katika umiliki na matumizi sahihi ya ardhi umepeklekea vijana wengi kuamini kuwa inahitajika uwe na pesa nyingi ili kumiliki ardhi jambo ambalo wadau wanasema si kweli ardhi inaweza kutumiwa na kumilikiwa na kila mtu .

Na Mariam Kasawa.
Ukosefu wa elimu na woga wa matumizi sahihi ya ardhi kwa vijana umepelekea vijana wengi kushindwa kutumia rasilimali za ardhi kujikwamua kiuchumi.

Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Youth Coalition (TYC) kupitia program ya boresha maisha ya vijana limeamua kutoa elimu kwa vijana juu ya fursa zinazo patikana katika umiliki na matumizi sahihi ya ardhi kupitia ufadhili wa WE effect.

Miriam Mwalimo na Daniel Masingija ni baadhi ya vijana ambao wamepata mafunzo hayo hapa wanasema mafunzo hayo yamewabadilisha mitazamo yao juu ya umiliki wa ardhi na wapo tayari kuwaelimisha vijana wengine juu ya faida za umliki na matumizi sahihi ya ardhi.

Sauti za vijana.
Picha ni moja kati ya vijana waliopata mafunzo hayo Miriam Mwalimo akiongea na Dodoma Tv.Picha na George John.

Lakini nini kiliwafanya Tanzania Youth Coalition (TYC) kujikita zaidi kwa vijana juu ya elimu hii ya umiliki na matumizi sahihi ya ardhi huyu hapa Bi Josephine Onesmo akitueleza.

Sauti ya Bi. Josephin Onesmo.

Wakati zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania hasa waishio vijijini wakitegemea kilimo, Utafiti wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha nchini (FSDT) umebaini kuwa wengi hawamiliki ardhi Zaidi ya nusu ya wananchi, asilimia 57, hawamiliki ardhi wanayoitumia kwa maana ya kutokuwa na nyaraka zinazohitajika kutokana na changamoto kadhaa zilizopo ikiwemo ukosefu wa elimu juu ya umiliki na matumizi sahihi ya ardhi.