Wananchi watakiwa kuacha kujichukulia sheria mkononi
14 August 2024, 5:14 pm
Jeshi la Polisi liendelee kutoa Elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa jamii kufuata misingi ya sheria.
Na Seleman Kodima.
Baadhi ya Wananchi wamesema kitendo cha kujichukulia sheria mkononi ni hatua mbaya hivyo wanaliomba jeshi la Polisi kuendelea kutoa Elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa jamii kufuata misingi ya sheria katika matukio yote yanayohitaji haki.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti wakazi hao kutoka halmashauri ya jiji la Dodoma kuhusu uwepo wa matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi nini kifanyike ili kupunguza vitendo hivyo.
Hapo jana Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limewataka Wananchi kuacha kujichukulia hatua mkononi badala yake watoe taarifa pindi wanapobaini kuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani.