Dodoma FM

TBA wafanikisha ujenzi wa Vihenge na maghala ya kisasa Nchini

7 August 2024, 6:36 pm

Picha ni Bw. Emmanuel Wambura meneja wa TBA Mkoa wa Dodoma akiongea na waandishi wa habari.Picha na Fred Cheti.

Mnamo July 16 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu alizindua mradi wa vihenge vya kisasa na maghala ya kuhifadhia chakula ambapo aliagiza kuongezwa kwa vihenge vingine.

Na Mariam Kasawa.
Serikali imeendelea kuwajali wakulima kwa kuhakikisha inajenga vihenge nchini kwaajili ya kuhifadhi mazao pamoja na mbegu.

Katika ujenzi huu wa Vihenge wakala wa Majengo Tanzania TBA ndio walipewa dhamana ya ujenzi huu.
Bw. Emmanuel Wambura meneja wa TBA Mkoa wa Dodoma anasema ujenzi wa vihenge hivi umelenga uhifadhi salama wa chakula na mbegu kwaajili ya wananchi na wao wamefanikiwa kwa asilimia 100 kukamilisha ujenzi huu katika mikoa kadhaa hapa Nchini.

Sauti ya Emmanuel Wambura meneja wa TBA Mkoa wa Dodoma
Picha ni moja ya Vihenge vya kisasa ambavyo vimejengwa na wakala wa majengo TBA . Picha na Fred Cheti

Mradi huo ambao ulianza 2019 nusu ya ujenzi wake tayari ilikwisha kamilika na kuzinduliwa na rais july 16 2024 kama anavyo eleza waziri wa kilimo mh. Hussein Bashe ambapo mgogoro uliotokea na mkandarasi, japokuwa tayari walikwisha tatua changamoto hizo.

Sauti ya Mh.Hussein Bashe .